Kula tangawizi mara kwa mara au kila siku kuna faida kadhaa za kiafya ikiwa ni pamoja na;
1.Kuimarisha mmeng'enyo wa chakula: Tangawizi husaidia mmeng'enyo wa chakula ,kupunguza gesi na kuvimbiwa
2.Kupunguza kichefuchefu: Tangawizi ina uwezo wa kupunguza kichefuchefu,ikiwa ni pamoja na kichefuchefu kinachotokana na ujauzito au kusafiri
3.Kuimarisha kinga mwilini: Tangawizi ina mchanganyiko wa antioxidants na virutubisho ambavyo husaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili na kupambana na magonjwa
4.Kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo: Tangawizi inaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo kwa kudhibiti shinikizo la damu na cholesterol
5.Kupunguza maumivu ya viungo: Inauwezo wa kupunguza maumivu ya viungo na misuli
6.Kupunguza dalili za mafua: Hupambana na dalili za awali za mafua zinazopelekea homa,maumivu ya mwili na kikohozi.Matumizi ya tangawizi husaidia kupunguza athari hizo na kufanya mtu ahisi vizuri kidogo
Tangawizi ni kiungo chenye nguvu za kiafya ambacho kimekua kikitumika kwa muda mrefu katika tiba asili.Fikiria kutumia tangawizi mara kwa mara ili kufurahia faida hizo zote kiafya.
Comments
Post a Comment