Sponsored Ad

Jinsi ya kusafisha mwili na kuboresha afya yako kwa kutumia detox ya asili


Detox ni nini?
Detox ni mchakato wa kuondoa sumu na uchafu mwilini kwa kutumia njia za asili kama vile vyakula,vinywaji na mazoezi.Mchakato huu husaidia mwili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuboresha afya yako kwa ujumla.

Faida za detox ya asili
1.Kuboresha mfumo wa mmeng'enyo: Detox husaidia kusafisha mfumo wa mmeng'enyo,kuondoa uchafu na sumu,na hivyo kuboresha usagaji wa chakula na kupunguza matatizo ya tumbo.

2.Kuongeza nishati: Kuondoa sumu mwilini kunasaidia kuongeza nishati na nguvu,kukufanya uwe na ufanisi zaidi katika shughuli zako za kila siku.

3.Kung'arisha ngozi: Detox husaidia kuondoa uchafu kwenye ngozi,hivyo huboresha mng'ao wa ngozi na kupunguza chunusi.

4.Kuimarisha kinga ya mwili: Detox husaidia kuboresha afya ya viungo muhimu kama ini na figo,na hivyo kuimarisha mfumo wa kinga na kupunguza hatari za magonjwa.

Jinsi ya kutumia detox ya asili 
Hapa kuna baadhi ya njia bora za kufanya detox ya asili nyumbani:

1.Maji ya limao na asali: Maji ya limao na asali ni mchanganyiko rahisi lakini wenye nguvu.Limao ina vitamini C na asidi ya citric ambayo husaidia kusafisha ini,wakati asali ina mali ya kupambana na bakteria.

Jinsi ya kutengeneza

.Chukua kikombe chenye maji ya uvuguvugu

.Ongeza juice ya limao nusu

.Ongeza kijiko cha chakula cha asali safi

.Koroga vizuri na unywe asubuhi kabla ya kula kitu chochote

2.Smooth ya kijani: Smooth ya kijani yenye mboga kama spinach,kabeji na matunda kama ndizi na parachichi,ni njia nzuri ya kupata virutubisho vyote muhimu kwa detox

Jinsi ya kutengeneza 

.Chukua spinachi safi

.Ongeza parachichi nusu

.Ongeza ndizi moja 

.Ongeza maji safi 

.Saga hadi upate mchanganyiko laini 

.Kunywa asubuhi kabla ya kula chochote

Anza leo kutumia detox ya asili mara kwa mara na uone tofauti kubwa katika afya yako na muonekano wako

 

Comments